Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka amesema Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Vijana itaendelea kuimarisha uratibu wa elimu ya uraia na uzalendo ili kuongeza ari ya vijana kupenda taifa na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
Amesema kuwa, hatua hiyo itahusisha uratibu wa majukwaa ya vijana katika ngazi ya mikoa na halmashauri, pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu ya uraia na uzalendo katika Halmashauri 184 nchini.
Vilevile, Mhe. Nanauka amesema kwamba Wizara itaendelea kuratibu mbio za Mwenge wa Uhuru na maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa, hatua inayolenga kukuza mshikamano, uzalendo na uwajibikaji miongoni mwa vijana.
Kadhalika, amesema Serikali itasimamia maadhimisho ya siku ya wanaojitolea kimataifa, siku ya vijana Afrika na siku ya vijana kimataifa, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ushiriki wa vijana katika shughuli za maendeleo ndani na nje ya nchi.
Aidha, amesisitiza kuwa juhudi hizo zinalenga kujenga kizazi cha vijana chenye maadili, uzalendo na utayari wa kushiriki katika shughuli za kijamii, kisiasa na kiuchumi za kuliendeleza taifa.
VIJANA Mkoa wa Singida wanatarajia kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba kutoka...
Wajasiriamali Mkoani Singida wameaswa kuziona changamoto zinazowakabili kama fur...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...