Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amekutana na kufanya kikao na vikundi vya vijana mkoani Katavi, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi mkoani humo, ambapo amesikiliza maoni yao na kueleza mikakati ya Serikali ya kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii.
Katika kikao hicho, vijana wamepongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kushughulikia changamoto zinazowakabili, hususan suala la upatikanaji wa mitaji kupitia mikopo isiyo na riba, pamoja na hatua mbalimbali zinazolenga kuongeza fursa za ajira na kujiajiri.

Vilevile, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maono ya kuanzisha Wizara inayosimamia masuala ya vijana, wakieleza kuwa hatua hiyo imeongeza kasi ya utekelezaji wa programu na sera zinazolenga maendeleo ya vijana nchini.
"Tunampongeza Rais wetu kwa maono makubwa ya kuanzisha wizara itakayoshughulikia changamoto zetu na kuleta suluhu ya matatizo ya vijana," amesema Israel Isanga, huku Yohana Masawe akipongeza utumishi wa Waziri Nanauka katika kusimamia agenda za maendeleo ya vijana.
Kwa upande wake, Waziri Nanauka amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua changamoto zinazowakabili vijana, ikiwemo kuboresha sera za maendeleo ya vijana, kuimarisha utoaji wa mikopo isiyo na riba, kuanzisha programu za uwezeshaji na kuwaunganisha vijana na fursa za kiuchumi zilizopo ndani na nje ya nchi. Aidha, amewahimiza vijana kujitokeza kutumia fursa hizo na kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya Taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka ames...
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe imenufauka na mradi wa shule mpya wenye thamani...