Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amepokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa uwezeshaji wa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya asilimia 10 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Halmashauri imeweka mikakati mbalimbali ya kuboresha utoaji wa mikopo hiyo, ikiwemo kutambua wananchi wanaostahili kunufaika, kubaini shughuli wanazozifanya, kusajili vikundi vyao vya ujasiriamali pamoja na kuvijengea uwezo kupitia mafunzo, kuwaunganisha na fursa za kiuchumi na kuwezesha kupitia mikopo isiyo na riba.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa mwaka wa fedha 2026/27 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imetenga jumla ya shilingi milioni 447.2 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo, ambapo shilingi milioni 119.2 zimetengwa kwa mikopo ya vijana, milioni 59.6 kwa wanawake, milioni 59.6 kwa watu wenye ulemavu na shilingi milioni 149 kwa ajili ya ujenzi wa soko la machinga litakalowawezesha wafanyabiashara wadogo kufanya shughuli zao katika mazingira bora.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Mhe. Nanauka ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwa usimamizi wa mpango wa mikopo ya asilimia 10 na kusisitiza umuhimu wa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia walengwa kwa wakati na kutumika katika shughuli za uzalishaji zitakazoinua kipato cha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka ames...
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe imenufauka na mradi wa shule mpya wenye thamani...