TANGAZO RASMI LA FURSA YA MKOPO WA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA
Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana (OR–MV) inapenda kuwatangazia vijana wote nchini kuwa dirisha la kupokea maombi ya mkopo kupitia program ya Shilingi Bilioni 200 ahadi ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalum limefunguliwa rasmi. Vijana wote wenye miradi au mawazo ya miradi wanakaribishwa kutuma maombi.