Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
Historia

Historia

Tarehe 10 Desemba, 2025 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisaini Hati ya idhini yenye kuonesha Mgawanyo wa Majukumu ya Mawaziri (Instrument) ya wizara 27. Hati hiyo ilitolewa kwenye tangazo Na. 685 la tarehe 19 Desemba, 2025. kwa mujibu wa tangazo hilo, Wizara imepewa dhamana ya usimamizi na utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Vijana, uratibu wa elimu ya uraia  na kujitolea kwa Vijana, ustawi wa Vijana, uwezeshaji wa vijana kiuchumi na uratibu wa majukwaa ya Vijana. Katika kutekeleza hayo, Wizara iliandaa mapendekezo ya Muundo na mgawanyo wa majukumu (Organization Structure) ambao upo katika hatua za ukamilishwaji.