Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana inashiriki “Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi ya Umma ambayo yameanza leo June 16, 2026 ‘Chinangali Park, Dodoma’.
Katika kuadhimisha wiki hiyo, vijana, wadau wa maendeleo ya vijana na wananchi kwa ujumla wanakaribishwa kutembelea banda la ofisi hiyo ili kupata huduma mbalimbali za kiutumishi.

Huduma zinazotolewa katika viwanja hivyo ni pamoja na elimu kuhusu fursa mbalimbali za vijana zinazopatikana katika ngazi za kikanda, kitaifa na kimataifa zinazotolewa na kuratibiwa na Wizara, elimu kuhusu uwezeshaji wa Vijana kiuchumi kupitia Mfuko wa Vijana, na elimu kuhusu fursa za uwezeshaji kwa Vijana kupitia Wizara za Kisekta.
Maadhimisho hayo yatakayohitimishwa Juni 23, 2026 yanabebwa na kaulimbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji jumuishi kwa huduma endelevu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka ames...