Na Byarugaba Innocent. Arusha
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Vijana Dkt.Kedmon Elisha Mapana leo Mei 4,2026 amefungua Mafunzo ya siku 4 kwa Watumishi wa Wizara hiyo yanayohusu utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 na Kanuni zake GN.No.518 ya Mwaka 2024
Mafunzo hayo muhimu ambayo ni nyenzo kiutendaji yanayofanyika kwenye Ukumbi wa hazina ndogo Jijini Arusha yamejikita kwenye historia ya sheria za Ununuzi wa Umma na Kanuni zake,Misingi mikuu ya Sheria ya Umma, Mamlaka zinazosimamia Ununuzi wa Umma, Mpangilio wa Kitaasisi,njia na taratibu za Ununuzi wa Umma,taratibu za zabuni, Usimamizi wa Mikataba, Uondoshwaji wa Mali na Mfumo wa Ununuzi (Nest)
Dkt.Mapana ametumia fursa hiyo kumpongeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Jenifa Omolo kwa kuwezesha mafunzo hayo muhimu yanayokwenda kuwajenga na kuwaimarisha kiutendaji hasa tunapoelekea kuanza kutekeleza bajeti ya Mwanzo ya Wizara ya Mwaka 2026/2027 kwa umakini zaidi
Aidha,Dkt.Mapana ametoa wito kwa Wakurugenzi wote kuwashirikisha watumishi wengine Kila wanapoandaa mafunzo ili kuwajengea uwezo mpana utakaowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi kwa manufaa ya Wizara na Taifa kwa ujumla
Mafunzo haya yanalenga kuwaboresha watendaji wa Wizara kuendelea kufanyakazi kwa kuzingatia weledi,Sheria,Kanuni na taratibu ili kuleta Matokeo chanya nchini
VIJANA Mkoa wa Singida wanatarajia kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba kutoka...
Wajasiriamali Mkoani Singida wameaswa kuziona changamoto zinazowakabili kama fur...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...