Wajasiriamali Mkoani Singida wameaswa kuziona changamoto zinazowakabili kama fursa za kuanzisha na kukuza biashara zenye tija kwa maendeleo yao na ya jamii.
Rai hiyo imetolewa Juni 3, 2026, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs), yenye lengo la kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa Mkoani humo na kukuza ushindani wake sokoni.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkufunzi wa Restless Development Bw. Simon Siliro, amesema mafanikio ya mjasiriamali yanategemea uwezo wa kutambua mahitaji ya jamii na kuyageuza kuwa fursa za kiuchumi akipongeza kuwa changamoto kama ukame zinaweza kuzaa fursa kupitia uwekezaji katika mazao yanayostahimili hali hiyo ikiwemo Alizeti, Mtama na Ulezi, pamoja na ufugaji wa nyuki kwa uzalishaji wa asali.
Aidha, Siliro amewasisitiza wajasiriamali kuboresha vifungashio vya bidhaa, kutafuta masoko mapya na kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na Serikali kukuza biashara zao.
_1780515586.jpeg)
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Mamalishe na Babalishe Tanzania (UMALITA) Mkoa wa Singida, Bi. Tatu Hamisi pamoja na kuwashukuru waandaaji wa mafunzo hayo ameongeza kuwa maarifa yaliyotolewa yatawasaidia wajasiriamali kuongeza tija na kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
VIJANA Mkoa wa Singida wanatarajia kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba kutoka...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka ame...