Vijana wana nafasi kubwa ya kuleta mageuzi ya kiuchumi, ikiwa watapata taarifa sahihi na kuchukua hatua. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka wakati alipotembelea Kikundi cha Vijana 'Tunathamini Afya Yako' kilichopo Majimoto, Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Kikundi hicho ambacho kwa sasa kina mradi wa duka la dawa za binadamu wenye thamani ya milioni 80, kati ya hizo milioni 50 ni mkopo kiliopewa na halmashauri kupitia mikopo ya asilimia 10.

Mhe. Nanauka amewataka vijana wengine kuiga mfano wa vijana wa kikundi hicho kwa kuwa wabunifu, na wenye uthubutu. Aidha, amesisitiza uaminifu miongoni mwa vijana wanaoungana na kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, hasa pale wanapopewa mikopo ya kukuza mitaji yao.
Katibu wa kikundi hicho, Rosemary Venance Soa ametoa shukrani kwa serikali, kwa kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mikopo isiyo na riba na amewasihi vijana wengine kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kujiajiri na kujiletea maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka ames...