Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro H. Mnyonge amewataka vijana kujitambua, kukubali kuelekezwa na kutimiza wajibu wao ili kuwawezesha kufikia ndoto zao na kuchangia maendeleo ya taifa.
Mhe. Songoro ameyasema hayo leo Aprili 14, 2026 wakati alipoongoza uzinduzi wa Jukwaa la Vijana “Vijana Platform” katika Manispaa hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kupokea Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Kinondoni.
Ili taifa liendelee linahitaji vijana wazalendo na wanaopenda taifa lao, na wenye ubunifu na dhamira ya kuliendeleza taifa lao kama alivyosisitiza baba wa taifa, Mwl. Nyerere kupitia falsafa yake ya ‘kujitegemea.’ Ameongeza Songoro.
Aidha, amebainisha kuwa, maendeleo ni mchakato wa muda mrefu hivyo amewataka Vijana kuwa na moyo wa uvumilivu wakati wa mchakato huo, ikiwa ni pamoja na kutafuta Suluhu ya matatizo yanayowakabili kwa njia ya mazungumzo.
“Kama kuna jambo linalokukera, kukuudhi au kuhisi linakuchelewesha, hakuna njia ya mkato. Tukae chini, tujadili, tutoe ushauri au maelezo yatakayotusaidia kusonga mbele.”
Vilevile, vijana wametakiwa kuenzi na kulinda umoja na mshikamano ambao umeachwa na waasisi wa taifa la Tanzania, ili kuwawezesha kufanya shughuli zao na kwa amani na utulivu na kujiletea maendeeleo pamoja na taifa kwa ujumla.
Shughuli zilizoambatana na uzinduzi wa Jukwaa la vijana katika Wilaya ya Kinondoni ni pamoja na vijana kupewa elimu kuhusu fursa ya tenda za serikali zinazopatikana kupitia PPRA; elimu ya uzalendo; na fursa za kiuchumi.
Uzinduzi wa Vijana Platform katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umehudhuriwa na vijana 700 kutoka makundi mbalimbali ya Wilaya hiyo, watumishi wa Manispaa, viongozi wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa na wadau mbalimbali wa masuala ya vijana.
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana Dkt. Kedmon Elish...
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Albert Gasper Msando ameongoza uzinduzi wa Jukwaa...
-Vijana waapa kudumisha uzalendo,Kuulinda Mwenge -Waziri Nanauka azidi ku...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Arthur Nanauka, ame...
-Rais Samia azindua minara 758 kuimarisha Mawasiliano Na Byarugaba Inno...