Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe imenufauka na mradi wa shule mpya wenye thamani ya milioni 342.9 ukihusisha ujenzi wa shule ya msingi na shule ya awali ambazo zinatarajia kupokea wanafunzi 420 kutoka shule jirani.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa shule hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo ni mwendelezo wa serikali kutimiza ahadi ya kuboresha miundombinu ya elimu, ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Waziri Nanauka amesema kuwa mradi huo umetekelezwa ili kusogeza huduma ya elimu karibu na makazi ya wanafunzi, ili kuwapunguzia umbali mrefu wa kufuata huduma ya elimu katika shule za vijiji jirani.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mkuu wa shule ya Majimoto, Seltus Mwanampemba ambaye ni msimamizi wa mradi huo ameeleza kuwa mradi huo uko kwenye hatua za ukamilishaji ambapo kwa sasa umekamilika kwa asilimia 95.
Wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa shule hiyo wameishukuru serikali kwa kutekeleza ujenzi wa mradi huo.
"Shule hii ni mkombozi kwa watoto wetu kwasababu itawapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shule" amesema Sophia Robert.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka ames...