KATIKA kuimarisha afya na utendaji kazi mahali pa kazi, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana (OR-MV) imetangaza kuanza rasmi kwa mazoezi ya kutembea kwa miguu kwa watumishi wake wote, kuanzia kesho tarehe 15 Mei, 2026.
Zoezi hili litakuwa likifanyika kila Ijumaa, kuanzia saa 10:00 jioni, ambapo watumishi wataanza safari kuanzia Makao Makuu ya Ofisi (HQ) kupitia Mji wa Serikali (Mtumba) hadi Barabara kuu ya Dar es Salaam.
Kuunga Mkono Jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan huu ni mwitikio wa moja kwa moja wa hamasa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akisisitiza mara kwa mara umuhimu wa watumishi wa umma na Watanzania kwa ujumla kufanya mazoezi.
Rais Samia amekuwa mfano bora katika kuhamasisha staili ya maisha yenye afya ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) na kuongeza tija katika kuwatumikia wananchi.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Edith Semtengo amesisitiza kuwa mazoezi ya kutembea yana faida lukuki, ikiwemo: Kuimarisha Afya ya Moyo, Kupunguza hatari ya shinikizo la juu la damu, Kupunguza msongo wa mawazo (stress) na kuchochea ubunifu kazini, Kujenga umoja na ushirikiano nje ya mazingira rasmi ya ofisi.
Aidha Bw. Abeid Lekey amesisitiza kuwa utamaduni huu kama Taasisi inayoshughulika na Maendeleo ya Vijana, unaenda kuwa mfano wa kuigwa kwa vitendo kitu ambacho kinadhihirisha kuwa watumishi wa umma wenye afya ndiyo injini kuu ya maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla.
Watumishi wote wanakumbushwa kuvaa mavazi ya michezo (tracksuits na raba) na kujitokeza kwa wingi.
“Mazoezi ni Afya – Tushiriki kwa Pamoja”
VIJANA Mkoa wa Singida wanatarajia kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba kutoka...
Wajasiriamali Mkoani Singida wameaswa kuziona changamoto zinazowakabili kama fur...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...