Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka amesema kupitia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Vijana aliyowasilisha leo Aprili 20, 2026 kuwa, serikali itaendelea kuimarisha ukuzaji wa biashara na uwezeshaji wa vijana kiuchumi ili kuongeza ajira na kipato kwa vijana nchini.
Mhe. Nanauka amesema kwamba serikali itaendelea kutoa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa vikundi vya vijana, sambamba na kutoa mikopo nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuwawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.
Vilevile, Mhe. Nanauka amesema Serikali itakarabati vituo viatatu vya mafunzo vya Sasanda, Ilonga na Marangu ili kutoa mafunzo ya muda mfupi katika sekta fani za kilimo biashara, TEHAMA na ujasiriamali.
Kadhalika, amesema Serikali inapanga kuanzisha vituo vya ubunifu kwa vijana (Vijana Hub) vitakavyowezesha kukuza ubunifu, kuendeleza vipaji, kutoa huduma za uratibu wa mawazo ya biashara, pamoja na kuwaunganisha vijana na fursa za masoko, teknolojia na mitaji kwa ajili ya kuongeza ushindani na tija katika shughuli zao za kiuchumi.
Aidha, amesema kwamba Serikali itaandaa mwongozo wa Kitaifa wa fursa za uwezeshaji kiuchumi ndani na nje ya nchi; kufanya mapitio ya Mwongozo wa utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa mwaka 2022; na kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa uwezeshaji utakaorahisha upatikanaji wa huduma kwa vijana.
VIJANA Mkoa wa Singida wanatarajia kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba kutoka...
Wajasiriamali Mkoani Singida wameaswa kuziona changamoto zinazowakabili kama fur...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...