Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka amezindua bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Usevya lenye thamani ya milioni 136.
Mhe. Nanauka amezindua bweni hilo akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kikazi aliyoanza mkoani Katavi tarehe 21 Julai, 2026.
Amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa bweni hilo na ametaka litunzwe kwa maendeleo endelevu ya shule hiyo na sekta ya elimu katika Halmashauri hiyo.
"Nawapongeza sana kwa kuwekeza katika elimu, kwa kutekeleza mradi huu katika viwango, kwasababu hiki ndicho ambacho Rais anasisitiza kuwa pesa zinapokuja zinapaswa kutumika kwenye miradi iliyokusudiwa."
Aidha, Mhe. Nanauka ameishukuru kampuni ya Barrick Tanzania kwa kushirkiana na serikali katika kufanikisha ujenzi wa bweni hilo. Aidha, ametoa wito kwa taasisi na kampuni nyingine kuiga mfano huo na kurudisha sehemu ya mapato yao kwa jamii, kwani ni takwa la kisheria.
Vilevile, amewataka wanafunzi kuwa na nidhamu katika masomo yao ili waweze kufanikiwa katika masomo yao na kutimiza ndoto. Kitakachokupeleka mbali si matokeo yako bali ni tabia nzuri, nidhamu na tabia njema" ameongeza Waziri Nanauka.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bweni hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Ndg. Shamim Daudi Mwariko ameishukuru serikali kwa kuendelea kutenga fedha za kuboresha miundombinu ya shule katika Halmashauri hiyo, kwani ni msingi muhimu wa kutoa elimu bora.
Kadhalika, Isack Charles ambaye ni mkazi wa Halmashauri hiyo amesema kuwa kukamilika kwa bweni hilo ni hatua muhimu katika kuendeleza ufaulu mzuri wa wanafunzi katika shule hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka ames...