Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana Dkt. Kedmon Elisha Mapana amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Vijana, kwa lengo la kuwawezesha kuwa Daraja la maendeleo ya taifa.
Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Vijana “Vijana Platform” katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, ambapo pia Dkt. Mapana ameeleza kuwa Wizara ya Maendeleo ya Vijana imeendelea kuweka mikakati ya kushugulikia masuala ya vijana ikiwemo kuanzisha Idara nne zitakazojihusisha na vijana moja kwa moja.
Vilevile, Dkt. Mapana amesema kuwa, kuanzishwa kwa Vijana Platform kunalenga kuwawezesha vijana kiuchumi, kuwapa nafasi ya kuchangia mawazo yao, kuwezesha kuundwa kwa baraza la vijana, kuwezesha vijana kuwa na taarifa sahihi kuhusu fursa za vijana zinazotolewa na serikali kupitia taasisi zake mbalimbali ikiwemo kupitia PPRA.
Kadhalika, Dkt. Mapana amewataka vijana kutumia shindano la ‘Vijana Uchumi Challenge’ kuwasilisha mawazo yao yatakayoleta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii katika nyanja mbalimbali.
Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Wizara ya Vijana ili kuratibu masuala ya vijana na kutatua changamoto zao kwa ufanisi zaidi.
VIJANA Mkoa wa Singida wanatarajia kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba kutoka...
Wajasiriamali Mkoani Singida wameaswa kuziona changamoto zinazowakabili kama fur...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...