Waziri Atembelea Kongani ya Vijana Bukoba, Awahimiza Kutumia Fursa Kujiletea Maendeleo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka ametembelea Kongani ya Vijana iliyopo Bukoba na kuwahimiza vijana kutumia ipasavyo fursa wanazozipata ili kujiletea maendeleo yao binafsi pamoja na kuchangia maendeleo ya taifa.
Katika ziara hiyo, Mhe. Nanauka alipata fursa ya kuzungumza na vijana wanaopata mafunzo katika kongani hiyo na kujionea shughuli mbalimbali za mafunzo ya stadi za kazi zinazotolewa kwa lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kujitegemea kiuchumi.
Akizungumza na vijana hao, Waziri Nanauka alisisitiza umuhimu wa mafunzo ya ufundi stadi katika kuwajengea vijana ujuzi wa vitendo utakaowawezesha kuanzisha shughuli za uzalishaji mali na kujipatia kipato.
Aidha, aliwahimiza vijana kuwa na nidhamu, kujituma na kutumia maarifa wanayoyapata kwa ubunifu ili waweze kufikia mafanikio katika maisha yao.
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Tanzania za kuendelea kuimarisha programu za maendeleo ya vijana na kuhakikisha wanapata ujuzi na fursa zitakazowawezesha kujenga maisha bora na mustakabali mzuri. 🚀
VIJANA Mkoa wa Singida wanatarajia kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba kutoka...
Wajasiriamali Mkoani Singida wameaswa kuziona changamoto zinazowakabili kama fur...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...