Kikundi cha vijana wajasiriamali kinachojulikana kama MALI HAI GROUP, kilichopo katika Kata ya Genge, Wilaya ya Muheza, Mkoa wa Tanga, ni miongoni mwa vikundi vya vijana vilivyonufaika na mikopo inayotolewa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
Kikundi hicho kinajishughulisha na shughuli za uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo thaluji (cement blocks), luvas, nguzo za mipaka, pamoja na uzalishaji wa miche ya miti na karavati. Kupitia shughuli hizo, kikundi kimeweza kujiongezea kipato, kuimarisha shughuli za kiuchumi za wanachama wake na kutoa mchango katika maendeleo ya jamii inayowazunguka.
Awali, kikundi hicho kilipatiwa mkopo wa kiasi cha Shilingi milioni 20 kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Muheza. Kutokana na matumizi sahihi ya mkopo huo na usimamizi mzuri wa mradi, thamani ya mradi kwa sasa imeongezeka na kufikia takribani Shilingi milioni 35.
Kesho, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii inatarajiwa kutembelea mradi huo uliopo Wilaya ya Muheza, Mkoa wa Tanga, kwa lengo la kujionea utekelezaji wa shughuli za kikundi hicho pamoja na mafanikio yaliyopatikana kupitia mikopo inayotolewa kwa vijana. Ziara hiyo inalenga pia kutathmini mchango wa miradi ya vijana katika kukuza ajira, uchumi wa vijana na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Vijana wa Muleba Wako Uso kwa Uso na Waziri wa Maendeleo ya Vijana Vijana kut...
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea kutoka kwa Waziri wa Fedha Balozi Kha...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, ikiongozwa na Mwenyek...