Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Hawa Mchafu Chakoma, leo tarehe 15 Machi 2026 imefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tanga kwa lengo la kutembelea na kukagua shughuli za mradi wa wajasiriamali unaotekelezwa na Kikundi cha Mali Hai Group, kikundi ambacho kiliwezeshwa kupitia mkopo wa mfuko wa maendeleo ya Vijana wa milioni 20
Katika ziara hiyo, wajumbe wa kamati walipata fursa ya kupokea maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Mali Hai Group kuhusu shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazotekelezwa na kikundi hicho, ikiwemo uzalishaji na ufugaji wa mali hai unaolenga kuwawezesha wanakikundi kujiongezea kipato na kuchangia maendeleo ya jamii inayowazunguka.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Hawa Mchafu Chakoma, alipongeza juhudi za kikundi hicho kwa ubunifu na ushirikiano wao katika kuendeleza shughuli za uzalishaji ambazo zimekuwa chanzo cha ajira na kipato kwa wanachama wake, hususan vijana.
Aidha, Kamati hiyo imeeleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa na mradi huo, huku ikisisitiza umuhimu wa kuendelea kuviwezesha vikundi vya wajasiriamali ili kuongeza tija katika uzalishaji, kukuza uchumi wa wananchi na kuimarisha maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Ziara hiyo ni sehemu ya jukumu la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii la kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na juhudi zinazolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Vijana wa Muleba Wako Uso kwa Uso na Waziri wa Maendeleo ya Vijana Vijana kut...
Kikundi cha vijana wajasiriamali kinachojulikana kama MALI HAI GROUP, kilichopo...
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea kutoka kwa Waziri wa Fedha Balozi Kha...