Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 29 ZACHANGISHWA KATIKA H...

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 29 ZACHANGISHWA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA PAG - KINYAMBURI.

20 Jun, 2026
ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 29 ZACHANGISHWA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA PAG - KINYAMBURI.

ZAIDI ya Shilingi Milioni 29 zimechangishwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Waasisi wa Pentekoste Tanzania (PAG), Jimbo la Hanang - Kinyamburi, Kata ya Dawari mkoani Manyara.

Akizungumza katika harambee hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo ameahidi na kuchangia jumla ya Shilingi Milioni 20 ikiwa ni mchango wa kuunga mkono juhudi za maendeleo ya taasisi za kidini nchini.

Mhe. Nanauka amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiroho, huku akipongeza umoja ambao umeonyeshwa na waumini na viongozi wa wilaya hiyo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Hanang’, Mhe. Asia Halamga, ameshiriki kikamilifu katika harambee hiyo na kufanikiwa kuchangisha jumla ya Shilingi Milioni 9 kutoka kwa waumini na wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wameuunga mkono harakati hizo za ujenzi.

Aidha Mhe. Nanauka ametumia fursa hiyo kuahidi kutembelea na kukutana na vikundi vya vijana jimbo la Hanang ili kuhamasisha ushiriki wao katika uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla.