-Awataka Vijana kujiamini, Serikali inathamini bunifu zao
-Mshindi kunyakua 50 Milioni
Na ORMV,Kibaha Pwani
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Vijana Dkt.Kedmon Elisha Mapana leo Julai 23,2026 amefungua rasmi kambi ya Vijana Uchumi Challenge inayoendelea kwenye Chuo cha uongozi cha Mwalimu Nyerere Kilichopo Kibaha Mkoani Pwani akielezea kuwa mwitikio wa Vijana 100 walioingia Kambi utaendelea kuweka historia katika Taifa.
Dkt.Mapana amesema kuwa jumla ya maombi 7852 yalipokelewa kutoka kwa Vijana wa Mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar yakidhirisha pasi na shaka kuwa Vijana Wana kiu ya kushiriki kujenga Uchumi wa Taifa ambapo 4,121 sawa na 52.5 asilimia yalikidhi vigezo vya Ushindani.
"Ubunifu wa Vijana umejikita zaidi katika TEHEMA na huduma za kidigitali kwa 30.7%, Teknolojia za Kilimo 27.8% huku Viwanda na biashara ikiwa na 21.3%"
Dkt.Mapana ameeleza kuwa lengo la Kambi ni kubadili mawazo ya ubunifu kuwa miradi inayowezekana kuwekezwa na kuwaandaa Vijana kufanya 'pitching' mbele ya wawekezaji na wadau wa Maendeleo.
Dkt.Mapana ameongeza kuwa lengo la serikali kupitia Wizara ni kujenga kizazi cha wabunifu si waombaji wa ajira,Vijana wanaotengeneza ajira na kukuza Uchumi wa Taifa.
Awali Mkurugenzi wa Biashara na uwezeshaji Vija Kiuchumi Edward Simon Haule amesema Dkt.Mapana aliweza kuibua Wazo la uwepo wa shindano hilo ambalo lilionekana kuwa gumu Kiutekelezaji lakini leo limetekelezwa kwa kishindo na Vijana na limedhihirisha kuwa Taifa lina Vijana wenye fikra pevu na bunifu zenye kuchangia kukuza pato na Maendeleo ya Taifa.
Dkt.Mapana ametoa rai kwa Vijana kujiamini wakati wa Pitching na kwamba Wazo la Kila kijana litalindwa na kufanyiwa kazi kwa manufaa ya Taifa.
Aidha,amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Vijana Bi.Jenifa Christian Omolo kwa kuridhia Mchakato Mzima wa Shindano la Vijana Uchumi Challenge tangu lilipozinduliwa rasmi Aprili,2026 na Mhe.Joel Arthur Nanauka na linatarajiwa kufikia tamati tarehe 6 Julai,2026 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre,Dar Es- ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan
Na OR-MV, Dodoma Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Vijana imeendelea na...
Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe...
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imeanza mazungumzo ya...
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Dkt. Kedmon Mapa...
ZAIDI ya Shilingi Milioni 29 zimechangishwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa...