Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imeanza mazungumzo ya kimkakati na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mtaji (UNCDF), yenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma za kifedha na fursa za kiuchumi kwa vijana nchini.
Hayo yamejiri leo Juni 22, 2026 katika kikao kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka na Katibu Mtendaji wa UNCDF, Bw. Pradeep Kurukulasuriya, ambapo wamejadili mikakati ya pamoja ya kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na ujasiriamali kupitia uwezeshaji wa kifedha.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Mhe. Nanauka amesema kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kushugulikia changamoto zinazokabili vijana kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuanzisha ushirikiano na taasisi za kifedha zikiwemo benki ili kuwawezesha vijana kupita mikopo nafuu.
“Tunatambua kuwa vijana ndio nguvu kazi kubwa ya taifa letu, hivyo tuna lengo la kujenga mfumo utakaowawezesha kupata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi ili kunufaika na fursa za maendeleo ya kiuchumi” ameyasema hayo Mhe. Nanauka.

Naye Katibu Mtendaji wa UNCDF, Bw. Kurukulasuriya amemhakikishia Waziri, Mhe. Nanauka kuwa UNCDF iko tayari kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Vijana ili kutafuta suluhu ya pamoja kuhusu changamoto za kiuchumi zinazokabili vijana, kupitia ufadhili wa kifedha.
Aidha Bw. Kurukulasuriya ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake za dhati kushugulikia changamoto za vijana, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikisha wataalamu wa maendeleo ya vijana ili kutekeleza programu za vijana kwa ufanisi.
Na OR-MV, Dodoma Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Vijana imeendelea na...
Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe...
-Awataka Vijana kujiamini, Serikali inathamini bunifu zao -Mshindi kunyakua 50...
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Dkt. Kedmon Mapa...
ZAIDI ya Shilingi Milioni 29 zimechangishwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa...