Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Dkt. Kedmon Mapana, amewataka vijana wanaosoma masomo ya sanaa nchini kuendelea kuyaenzi na kuyatumia kama nyenzo ya kujiletea maendeleo binafsi na ya taifa badala ya kukata tamaa kutokana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika safari yao ya taaluma.
Dkt. Mapana ametoa rai hiyo leo Juni 20, 2026, alipokuwa akizungumza na mamia ya vijana waliojitokeza kushiriki Tamasha la Sanaa Blast Festival, lililoandaliwa na Idara ya Sanaa Bunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kufanyika katika viunga vya chuo hicho.
Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Christian Makonda, Dkt. Mapana alisema sekta ya sanaa na ubunifu imeendelea kuwa moja ya maeneo yenye fursa kubwa za ajira, uwekezaji na ukuaji wa uchumi, hivyo vijana wanapaswa kujiamini na kuendeleza vipaji vyao.

Alisisitiza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha vijana wabunifu kutumia vipaji na maarifa yao kujiajiri, kuajiri wengine na kuchangia maendeleo ya taifa kupitia uchumi wa ubunifu.
Aidha, aliwataka vijana kutumia teknolojia za kidijitali kutangaza kazi zao, kupanua masoko na kuongeza thamani ya bidhaa na huduma zinazotokana na ubunifu wao, huku akibainisha kuwa dunia ya sasa inatoa fursa nyingi kwa wabunifu wanaotumia maarifa na teknolojia kwa ufanisi.
Tamasha hilo limewakutanisha wanafunzi, wasanii, wabunifu na wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa kwa lengo la kuonesha vipaji, kubadilishana uzoefu na kuhamasisha ubunifu miongoni mwa vijana nchini.
Na OR-MV, Dodoma Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Vijana imeendelea na...
Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe...
-Awataka Vijana kujiamini, Serikali inathamini bunifu zao -Mshindi kunyakua 50...
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imeanza mazungumzo ya...
ZAIDI ya Shilingi Milioni 29 zimechangishwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa...