Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Bi. Jenifa Christian Omolo, leo Juni 11, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya NMB ukiongozwa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Bw. Filbert Mponzi. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, Jijini Dodoma.
_1781206905.jpeg)
Mazungumzo hayo yamelenga kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana na Benki ya NMB, hususan katika kuwawezesha vijana kiuchumi, kuimarisha ujumuishi wa kifedha na kukuza fursa za maendeleo kwa vijana nchini.
Aidha,viongozi hao wamejadili namna bora ya kuimarisha ushirikiano utakaowezesha vijana wengi zaidi kunufaika na huduma za kifedha, fursa za ujasiriamali na programu mbalimbali za maendeleo zinazochochea ukuaji wa uchumi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, am...
Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, wizara za kisekta, s...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, am...
“Tunataka kijana apate msaada mapema, karibu na mazingira yake, kwa namna...
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...