Facebook
Instagram
Youtube
Barua Pepe
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Wasiliana nasi
Mrejesho
ENG
SWA
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
Mwanzo
Kuhusu Sisi
Kuhusu Sisi
Kuhusu Wizara
Dira
Dhima
Majukumu Yetu
Maadili ya Msingi
Utawala
Utawala
Muundo wa Utawala
Menejimenti
Vitengo
Idara
Machapisho
Machapisho
Ripoti
Fomu
Makala
Sheria
Kanuni
Nyaraka Zengine
Huduma Mtandao
Huduma Mtandao
e-Mrejesho
Ofisi Mtandao
Kituo cha Habari
Kituo cha Habari
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maktaba ya Video
Maktaba ya Picha
Hotuba
Mabango
Kituo cha Simu
Maktaba ya Picha
Ukumbi wa Habari
Maktaba ya Picha
Picha
SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUPITIA VIJANA PLATFORM .
Waziri Nanauka Awagusa Vijana Wenye Ulemavu katika Jukwaa la Vijana Mtwara Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amewagusa na kuwapa matumaini vijana wenye ulemavu wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Vijana (Vijana Platform) lililofanyika katika Mkoa wa Mtwara. Katika tukio hilo, Mhe. Nanauka alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa vijana wote, wakiwemo vijana wenye ulemavu, wanapata fursa sawa za kushiriki katika shughuli za maendeleo, elimu, ujasiriamali na ajira. Alieleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mikakati na mazingira rafiki yatakayowawezesha vijana wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa. Aidha, Waziri Nanauka aliwahimiza vijana hao kujiamini, kutumia vipaji na ujuzi walionao pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia programu za uwezeshaji wa vijana. Kwa upande wao, vijana wenye ulemavu walieleza kufurahishwa na hatua ya Serikali ya kuwajumuisha katika majukwaa ya vijana, wakisema kuwa jukwaa hilo limewapa nafasi ya kusikilizwa, kueleza changamoto zao na kushiriki katika kupanga mikakati ya maendeleo yao.
‹
1
2
›