Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
Matangazo

TANGAZO LA FURSA KWA VIJANA – USHIRIKI OCC11 (MOMBASA, KENYA)

04 May, 2026

Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana (OR-MV) inakaribisha maombi kutoka kwa vijana Watanzania kushiriki Jukwaa la Uongozi la Vijana (14–15 Juni 2026) sambamba na Mkutano wa 11 wa Bahari Yetu (OOC11).

Tunatafuta vijana (miaka 18–35) wenye taaluma/uzoefu katika: Sayansi ya Bahari/Oceanography, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, Uvuvi na Aquaculture, Uchumi wa Buluu, Sheria za Mazingira/Bahari, Sera za Umma/International Relations, GIS/Data Science, au Usalama wa Bahari. Kipaumbele kitatolewa kwa wenye uzoefu wa vitendo kwenye miradi ya bahari/mazingira, hasa kutoka mikoa ya pwani, na wenye uwezo wa kuiwakilisha Tanzania kimataifa.

Jinsi ya Kuomba:

Tuma CV pamoja na barua fupi ya motisha kupitia barua pepe: nassibu.mwaaifunga@vijana.go.tz
Kichwa cha barua: “Application – OCC11 Youth Delegate”

Kwa maelezo zaidi, wasiliana kupitia simu: 0716 421 160

Mwisho wa kupokea maombi ni Jumanne, tarehe 04/05/2026