Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
Matangazo

TAARIFA KWA UMMA

16 Mar, 2026

Wizara ya Maendeleo ya Vijana inapenda kuwataarifu vijana nchini kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana inaendelea kutoa mikopo kwa vijana ili kuwawezesha kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Mikopo hiyo inalenga kusaidia vijana wajasiriamali kuanzisha au kupanua miradi katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara ndogo na za kati, pamoja na uzalishaji wa bidhaa na huduma. Lengo la mpango huu ni kuongeza fursa za ajira, kukuza kipato cha vijana na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.

Vijana wanahimizwa kuunda au kujiunga na vikundi vya uzalishaji, kuandaa miradi yenye tija na kuwasilisha maombi ya mikopo kupitia mamlaka husika katika ngazi za halmashauri au ofisi zinazoshughulikia maendeleo ya vijana.

Wizara inaendelea kuwahimiza vijana kutumia ipasavyo fursa hii ya mikopo, kusimamia vyema miradi yao na kuhakikisha marejesho yanafanyika kwa wakati ili kuwezesha vijana wengine kunufaika na mfuko huo.

Kwa taarifa zaidi kuhusu namna ya kupata mikopo hiyo, vijana wanashauriwa kufuatilia matangazo rasmi ya Wizara ya Maendeleo ya Vijana pamoja na mitandao ya kijamii ya taasisi husika.